1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umuhumi wa wafanyi tafsiri

2 Mei 2017

Wakalimani wana kazi muhimu ya kuzitunza lugha mbambali duniani, kazi zao zimewezesha lugha zinazozungumzwa 6000 hadi 7000 kuendelea kuwepo na lahaja adimu 3000 bado kuendelea kuwepo

https://p.dw.com/p/2cF1P
TransStar Projekt Ukraine Claudia Dathe
WakalimaniPicha: DW

"Bila ya tafsiri, hakuna kumbukumbu ya binadamu,"  alisema mwana isimu Astrid Guillaume wa chuo kikuu cha Sornonne cha Paris. "Tunajua historia na utamaduni wa sehemu mbalimbali duniani kutokana na tafsiri," aliongezea kusema.

"Neno "translate" yaani tafsiri linatokana na neno la kilatini ambalo ni "traducere" lenye maana ya kusambaza. Hii hapa mifano mitatu ya jinsi gani tafsiri inaleta uanuwai wa kiisimu.

Rozenn Milin ni mzaliwa wa familia ya wakulima wadogowadogo katika mji wa Brittany, magharibi mwa Ufaransa, ambako wanazungumza Breton. Rozenn angeweza kuwa mkalimani wa lugha ya kifaransa na kibreton. Lakini badala yake aliamua kufanya tafsiri ya lugha ambazo ni adimu sana duniani kupitia mradi wake.

Sorosoro maana yake ni pumzi, hutuba na lugha katika lugha ya Araki ambayo ni lugha iliyopo hatarini kupotea na sasa inazungumzwa na watu kumi tu. Ni moja ya lugha znazotumiwa katika visiwa vya Pasifiki vya Jamhuri ya Vanuatu.

Lengo la mdasi wa Sorosoro

Lengo la mradi huu wa Sorosoro ni kuzihifadhi lugha ambazo ziko hatarini kupotea kwa njia ya kuwarikodi watu ambao bado wanazungumza lugha hizi na baadaye kuzihifadhi  katika chuo cha sauti na picha cha Ufaransa.

"Wakalimani wana kazi muhimu katika mradi huu unaotafsiri hadithi za filamu, nyimbo na sherehe za ibada," alisema Milin.

Katika upande wa lugha za ishara, kuna lugha nyingi sana za ishara kama zilivo nchi mbalimbali.

Hakuna lugha ya ishara ya kimataifa.

"Lakini hakuna kitu muhimu kama kufahamu na kujieleza lugha yako mwenyewe kupitia lugha ya ishara," alisema makamu wa rais wa chama cha viziwi cha Ufaransa cha FNSF Ronit Leven.

 Katika zama hizi za teknolojia, kumekuwa na upotofu wa tafsiri kupitia tafsiri za kwenye mtandao kama vile tafsiri ya google. Katika kitabu chake cha 2017 "Google Moi" au "nigoogle mie" mwanafalsafa Barbara Cassin aliandika vipi sentensi ya biblia "na Mungu alimuumba binadamu kwa mfano wake" imefanyimwa tafsiri kwa kijerumani na kifaransa mara kadhaa kupitia mtandooni na tafsiri ya google imetafsiri: "na binadamu kupitia sura yake katengeneza mungu."

Screenshot Google Translate Deutsch Englisch
tafsiri ya mtandaoni ya googlePicha: DW/D. Fong

"Lakini sasa kuna jitihada za kujaribu kurekebisha tafsiri za mtandaoni. Na sasa tafsiri kama hiyo hapo haiwezi kutokea, matokeo ya tafsiri za mtandaoni ni mazuri na yanaweza kutumika," alisema Cassin akizungumzia kazi yake mwenyewe inayoitwa Eulogy of translations yaani taabini ya tafsiri.

Ubora wa tafsiri utazidi kuimarika kutokana na maendeleo ya sekta ya ubunifu wa kiteknolojia kwa kuigiza ubongo wa binadumu jinsi unavyofanya kazi. Mfumo kama huo ulizinduliwa na kampuniya Kifaransa ya SYSTRAN, ambayo ni muazishi pia wa tafrisi za moja kwa moja ta mtandaoni.

Mwandishi: Najma Said/AFPE

Mhariri:Iddi Ssessanga