SiasaIran
Wakaguzi wa IAEA wamewasili Iran
22 Februari 2023Matangazo
Afisa huyo mwandamizi amesema wakaguzi hao tangu Jumanne wamekwishaanza kazi ya majadiliano na ukaguzina kwamba utata uliosababishwa na wakaguzi umetatuliwa.
Juma lililopita shirika hilo la Umoja wa Mataifa lenye kuratibu shughuli za nyuklia lilisema lipo katika majadiliano na Iran.
Mazungumzo hayo yalikuwa yanafanyika kutokana na matokeo ya hivi karibuni baada ya shirika la habari la Bloomberg kuripoti madini ya urani yamerutubishwa kwa kiwango cha asilimia 84, kikiwa karibu na uundwaji wa silaha za nyuklia.