Raia wanaoishi kwenye maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa M23 mkoani Kivu Kaskazini huko Kongo wanashuhudia ongezeko la ukosefu wa chakula hali inayosababisha njaa tangu waasi hao walipoyageuza mashamba yao kuwa maeneo ya mapigano kati yao na jeshi la serikali ya Kongo. Hali hiyo inayoiathiri miji mikuu kama Goma na Bukavu, imekuwa ni kitisho kikubwa kwa wananchi. Msikilize Benjamin Kasembe.