Makubaliano ya kusitisha uchafuzi wa taka za Plastiki bado
1 Desemba 2024Mataifa ya dunia, yanayoshiriki mazungumzo yamekuwa yakijaribu tangu jana kufikia makubaliano katika vikao vya faragha lakini rasimu ya mkataba iliyotolewa imeamuwa suala hilo lijadiliwe katika kikao cha wazi baadae leo.Rasimu hiyo inapendekeza uwezekano wa kupigwa marufuku baadhi ya bidhaa za plastiki za kutumika mara moja au zinazotowa kemikali za sumu. Panama na Fiji zimetaka mataifa ambayo hayaungi mkono malengo ya rasimu hiyo yajiweke pembeni,msimamo ambao umeungwa mkono na Mexico,Ufaransa,Rwanda na Umoja wa Ulaya ambazo zimesema kwa pamoja zitafanya kila ziwezalo kushinikiza rasimu hiyo ipitishwe kutatua mgogoro wa uchafuzi unaosababishwa na taka za plastiki.Ghana imeiita rasimu hiyo ya sasa kuwa dhaifu Kumi,ambayo haizilazimishi nchi kusitisha kabisa matumizi ya bidhaa za plastiki.