Wajue wachezaji waliochaguliwa na Loew
Licha ya wasiwasi kuhusu kushiriki kwao, Manuel Neuer, Ilkay Guendogan na Mesut Oezil wamechaguliwa, wakati Mario Goetze ni miongoni mwa majina makubwa yaliyoachwa nje.
Manuel Neuer
Je, kipa bora zaidi wa Ujerumani atakuwa katika hali nzuri kucheza? Hata ingawa Neuer hakucheza katika sehemu kubwa ya msimu kwa kuwa majeruhi, Joachim Löw amemjumuisha nahodha wake huyo kikosini akitaraji kuwa atapona kikamilifu.

Mechi za Kimataifa: 74 / Mabao: 0 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 2
Marc-André ter Stegen
Kipa huyo wa Barcelona amekuwa chaguo la Löw wakati Neuer akiwa mkekani. Huku nahodha wa Ujerumani akiwa amerejea, ter Stegen huenda akarejea tena kwenye benchi, lakini pia huenda pia akaanza katika kikosi cha kwanza wakati Neuer akiyanoa makali

Mechi za kimataifa: 19 / Mabao: 0 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0
Bernd Leno
Kipa huyo wa Leverkusen shot stopper ni mwingine katika kikundi cha makipa wa Ujerumani. Ijapokuwa amekuwa na msimu mzuri, yuko nyuma ya Neuer na ter Stegen katika msimamo wa ubora.

Mechi za kimataifa: 6 / Mabao: 0 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0
Kevin Trapp
Trapp ndiye aliyenufaika sana na pengo la Neuer kuwa nje. Hakuwa mafanikio mengi sana msimu uliopita, aliichezea Paris Saint-Germain mechi 12 tu na kufanya makosa kadhaa makubwa. Lakini amechaguliwa kwa sasa.

Mechi za kimataifa: 3 / Mabao: 0 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0
Jerome Boateng
Mchezaji huyo wa Bayern Munich ndiye beki bora zaidi wa Ujerumani, na mmoja wa majina ya kwanza kwenye orodha ya Loew. Lakini Boateng alipata maumivu ya paja dhidi ya Real Madrid mwezi Machi, na kutilia shaka kama atakuwa shwari kucheza Kombe la Dunia.

Mechi za kimataifa: 70 / Mabao: 1 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 2
Mats Hummels
Anashirikiana na Boateng katika safu ya ulinzi katika klabu na timu ya taifa na ni mmoja wa wachezaji muhimu wa Loew. Swali sio kama atakuwa katika timu ya kwanza katika Kombe la Dunia, lakini nani ataanza na yeye.

Mechi za Kimataifa: 63 / Mabao: 5 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 1
Antonio Rüdiger
Beki huyo wa Chelsea anaaminiwa na Loew, maana ameshirikisha katika mechi zote za kufuzu katika dimba la Dunia. Huenda kimsingi akawa mchezaji wa akiba kwa Boateng na Hummels.

Mechi za kimataifa: 23 / Mabao: 1 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0
Jonathan Tah
Mchezaji huyo wa Bayer Leverkusen huenda akawa mbadala kukiwa na majeruhi. Tah, mwenye umri wa miaka 22 alikuwa na msimu wa matatizo ya majeraha kwa Leverkusen, lakini anaonekana kuwa mchezaji wa usoni. Hata hivyo, huenda akawa mmoja wa majina manne yatakayoachwa ifikapo Juni 4 wakati timu itapunguzwa hadi 23.

Mechi za kimataifa: 3 / Mabao: 0 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0
Niklas Süle
Alikuwa na msimu mzuri wa kwanza katika klabu ya Bayern na ana uzoefu wa kucheza pamoja na Hummels na Boateng. Süle mwenye umri wa miaka 22 sasa anatarajiwa kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.

Mechi za Kimataifa: 9 / Mabao: 0 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0
Matthias Ginter
Uhamisho wake kutoka Borussia Dortmund hadi Borussia Mönchengladbach hakujaathiri kabisa nafasi za Ginter katika timu ya taifa. Mchezaji huyo wa akiba ndiye alikuwa mdogo zaidi katika kikosi cha 2014, lakini hakucheza hata dakika moja katika dimba hilo. Atatumai kucheza mara hii lakini huenda pia akaachwa nje.

Mechi za kimataifa: 17 / Mabao: 0 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 1
Joshua Kimmich
Beki huyo wa Bayern sio tu beki bora zaidi wa kulia katika timu ya Ujerumani, lakini pia mmoja wa mabeki bora zaidi wa kulia duniani. Loew atamhitaji akiwa kwenye hali yake bora zaidi katika Kombe la Dunia.

Mechi za kimataifa: 27 / Mabao: 3 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0
Jonas Hector
Atacheza katika ligi ya daraja la ili msimu ujao baada ya Cologne kushushwa ngazi kutoka Bundesliga. Kabla ya hapo, Hector anatarajiwa kucheza katika Kombe la Dunia kwa mara yake ya kwanza akiwa beki wa kushoto.

Mechi za kimataifa: 36 / Mabao: 3 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0
Marvin Plattenhardt
Licha ya kucheza kwa maa ya kwanza katika timu ya taifa kwenye Kombe la Mabara mwaka jana, mchezaji huyo wa Hertha Berlin anajikuta katika nafasi nzuri ya kwenda Urusi. Mchezaji huyo mwenye umri wa 26 anaweza kuwa wa akiba katika nafasi ya Hector.

Mechi za kimataifa: 6 / Mabao: 0 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0
Toni Kroos
Kroos anatarajiwa kuwa nguzo muhimu katika safu ya kiungo ya mabingwa hao watetezi. Kiungo huyo wa The Real Madrid amekuwa akichaguliwa moja kwa moja katika timu ya Ujerumani kwa muda sasa.

Mechi za kimataifa: 82 / Mabao: 12 / Mashindano Kombe la Dunia: 2
Sami Khedira
Akiwa na umri wa miaka 31, kiungo huyo wa Juventus huenda asiwe katika kiwango chake bora. Lakini uongozi wake ndio anaoupenda na uwepo wake uwanjani utafanya bila shaka achaguliwe katika timu ya taifa.

Mechi za kimataifa: 73 / Mabao: 7 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 2
Sebastian Rudy
Alikosa kushiriki katika Kombe la Dunia la 2014 nchini Brazil na katika Euro 2016 nchini Ufaransa. Baada ya kuanza katika kila mechi za Kombe la Mabara 2017, Rudy anajaribu kumshawishi Loew hatimaye kumleta katika mashindano makubwa.

Mechi za kimataifa: 24 / Mabao: 1 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0
Ilkay Gündogan
Kiungo huyo wa Manchester City hatimaye yuko hali nzuri baada ya kukosa mashindano mawili makuu kutokana na majeraha tofauti. Ni kiungo anayekaa nyumasana na anayeweza kufanya mambo kuwa sawa katikati mwa uwanja

Mechi za kimataifa: 24 / Mabao: 4 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0
Mesut Özil
Kiungo huyo wa Arsenal ni mmoja wa wachezaji bora wabunifu duniani, lakini mara kwa mara anakosolewa kwa kile kinachoonekana kupotea katika mechi au nyakati muhimu. Atakuwa mmoja wa wachezaji wa Loew nchini Urusi

Mechi za kimataifa: 89 / Mabao: 22 / Kombe la Dunia: 2
Thomas Müller
"Müller hucheza kila mara," kocha wa zamani wa Bayern Louis Van Gaal alisema wakati mmoja. Sio mshambuliaji katika hali halisi, lakini kawaida yeye huonekana kujua namna ya kufunga mabao. Ana uzoefu wa Kombe la Dunia pia. Alikuwa mfungaji bora wa Kombe la Dunia 2010 na akawa wa tatu 2014.

Mechi za kimataifa: 90 / Mabao: 38 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 2
Marco Reus
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 hatimaye anaonekana kuwa atacheza dimba lake la kwanza la Dunia. Anapaswa tu kukamilisha mazoezi yake katika kambi ya Tyrol bila kujiumiza mwenyewe...

Mechi za Kimataifa: 29 / Mabao: 9 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0
Julian Draxler
Mchezaji mwingine anayependwa na Loew, Draxler alikuwa nahodha wa Ujerumani katika Kombe la Mabara mwaka jana. Baada ya kutopata muda wa kutosha wa kucheza katika timu yake ya Paris Saint-Germain msimu huu, Draxler analenga kuichukua nafasi yake katika kiwango cha kimataifa.

Mechi za kimataifa: 42 / Mabao: 6 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 1
Leon Goretzka
Kiungo huyo mpya wa Bayern Munich alionyesha mchezo mzuri katika Schalke msimu huu, baada ya kutamba katika Kombe la Mabara mwaka jana. Hata hivyo huenda akawekwa kwenye benchi wakati mastaa wa Ujerumani watakaporudi kikosini.

Mechi za kimataifa: 14 / Mabao: 6 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0
Leroy Sané
Kasi huenda likawa jina la katikati la Leroy Sané. Atampa Loew kasi na ujuzi kwenye eneo la pembeni mwa uwanja baada ya kushinda taji la Ligi ya Premier Manchester City.

Mechi za kimataifa: 11 / Mabao: 0 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0
Julian Brandt
Winga huyo mwenye umri wa miaka 22 alipewa majukumu zaidi katika timu ya Leverkusen msimu huu. Sasa analenga kuiimarisha nafasi yake katika timu ya Loew kwa miaka ijayo.

Mechi za kimataifa: 14 / Mabao: 1 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0
Timo Werner
Mshambuliaji huyo wa Leipzig ni mdogo, mwenye kasi na mwenye nguvu tofauti na walivyo washambuliaji wengine wa Ujerumani. Mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 22 anaonekana kuwa mshambuliaji nambari moja wa Loew baada ya kushinda tuzo ya mfungaji bora katika dimba la mwaka jana la Kombe la Mashirikisho.

Mechi za kimataifa: 12 / Mabao: 7 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0
Mario Gomez
Mshambuliaji huyo wa Stuttgart ameshuka chini katika orodha ya ubora tangu alipotamba sana katika Euro 2016. Hata wakati akiwa na umri wa miaka 32, bado ni mmoja wa wafungaji bora wa Ujerumani. Lakini anapaswa kuwa katika hali nzuri ili kumshawishi Loew ampeleke Urusi.

Mechi za kimataifa: 73 / Mabao: 31 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 1
Nils Petersen
Mshambuliaji huyo wa Freiburg amewashangaza wengi kwa kujumuishwa katika kikosi cha Loew licha ya kumaliza msimu wa Bundesliga akiwa mfungaji mwenza bora wa Ujerumani akiwa na mabao 15. Petersen hajawahi kuichezea timu ya taifa, lakini atalenga kuisahau penalti aliyopoteza katika Michezo ya Olimpiki mwaka wa 2016

Mechi za Kimataifa: 0 / Mabao: 0 / Mashindano ya Kombe la Dunia: 0