Wananchi wa Ujerumani kwa kiasi kikubwa wanaunga mkono masharti mapya yaliyoanza kutekelezwa Jumatano ili kupambana na maambukizi ya virusi vya corona yaliyoongezeka nchini humo. Utafiti uliofanywa na YouGov umeonyesha asilimia 73 ya wajerumani wanaunga mkono uamuzi wa kufungwa kwa baadhi ya shughuli pamoja na shule. #KurunziUjerumani