Waislamu washerehekea sikukuu ya Idd el-Hajj.
19 Desemba 2007Mecca, Saudi Arabia.
Leo ni sikukuu ya idd el-Hajj. Mamilioni ya waislamu duniani kote wanasherehekea sikukuu hii ya Idd ul-adhah.
Mamilioni ya Waislamu jana wameadhimisha kilele cha ibada ya Hija ya kila mwaka kwa kukaa katika mlima Arafat.
Katika maeneo ya Afrika mashariki na kati leo nchi za Kenya , Uganda, Burundi na jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo wanasherehekea sikukuu hii. Wakati huo huo Waislamu mahujaji leo walikuwa wanatekeleza tukio la kutupa vijiwe katika nguzo nje kidogo ya mji wa Mecca, kunyoa nywele na kununua wanyama wa kuchinja , ikiwa ni siku ya tatu ya ibada ya kila mwaka ya Hijja.
Wengi waliwasili hapo baada ya kutembea kwa miguu kwa upamba wa kilometa 20 wakati wa usiku, wakipumzika tu kwa kulala kwa saa chache katika eneo la Muzdalifa, ambako walikusanya kila mmoja kiasi cha vijiwe 49.