Wairan kutumia mitandao kutoa maoni ya kisiasa
19 Mei 2017Iran itachaguwa rais wake mpya hapo kesho Ijumaa tarehe 19 mwezi wa Mei, na hali katika mitandao ya kijamii inazidi kupamba moto. Kama ilivyo kawaida ya nchi nyingi ambazo zinadhibiti utumiaji wa mitandao ya kijamii na vyombo vya habari wakati wa uchaguzi, Iran sasa imepata uhuru wa muda mfupi wa kujieleza. Juu ya yote, watumiaji wa mitandao ya kijamii wanachukua nafasi hiyo kuelezea mawazo yao, na mahitaji juu kwa wagombea.
Wanasiasa pia wanatumia mitandao ya kijamii kama njia ya kuhamasisha wapiga kura. Mapema Mwezi huu wa Mei, Kiongozi mkuu wa kidini Khamenei, mtumiaji wa mara kwa mara wa Twitter, alitoa wito kwa Wairani wote kutumia haki yao ya kupiga kura. Khamenei alisisitiza kwamba wapigakura wajitokeze tarehe 19 Mei ili wathibitishe mfumo wa kisiasa wa Iran.
Khamenei aliandika ifuatavyo katika mtandao wake wa twitter: Jamhuri ya kiislamu msingi wake ni kura ya watu. Uislamu unatuambia tufuate njia ya watu kupiga kura.
Hamu kwa ajili ya elimu ya siasa
Kipindi kabla cha uchaguzi kinatoa fursa kuu kwa wanaharakati mtandaoni kugundua unyanyasaji na kutekeleza malengo ya muda mrefu.
"Tunaona kuwepo kwa hamu kubwa juu ya elimu ya siasa. Na huo ndio mwenendo unaoonekana katika mitandao ya kijamii," mwanaharakati wa haki za binadamu na muandishi wa habari Reza Haghighatnejad aliliambia shirika la habari la Deutsche Welle.
Mwanaharakati huyo amekuwa akichunguza shughuli za mitandao ya jamii za Wairan na matumizi yao ya mtandao.
"Wengi wao wanataka kuburudishwa. Ukweli ni wengi wao hawana mvuto hasa katika maswala ya siasa. Lakini kinachotupa tamaa ni uongezekaji wa watumizi wa mtandao kushiriki katika kampeni wakiwa na malengo ya muda mrefu," alisema Reza.
Maslahi ya ghafla katika haki za wanawake
Masuala kama hayo ya kijamii sio tu kupokea msaada mpana katika mitandao ya kijamii, lakini pia wanawake wamekuwa mandhari ya kampeni kwa wagombea wa urais.
" Tunawaona wagombea wa uraisi ghafla wametambua umuhimu wa haki za wanawake na masuala ya haki za raia. Ni wakati wa kupaza sauti ambao unaweza kukufanya wewe ukaamini kuwa wako na wapinzani," alisema mchunguzi wa mambo ya jinsi katika chuo kikuu cha Toronto Victoria Tahmasebi-Birgani."
Birgani amesema kuwa wagombea wote ni wanachama wa mfuno wa siasa wa nchi hiyo, na mfumo huo unawakilisha wanaharakati wa haki za wanawake. Lakini pia mitandao ya kijamii imefanya kuwa haiwezekani kutogusia suala la uhuru na usawa wa jamii.
Iran ni nchi yenye vijana wengi,na wengi wakiwa katika rika la miaka 30. Asilimia 80 ya wairain wanaweza kusoma na kuandika. Iran inatilia sana umuhimu wa elimu, lakini elimu ya siasa nikama haipo mashuleni na katika vyuo vikuu. Vyombo vya habari ni vya serikali au vinadhibitiwa vikali.
"Kituo cha radio na televisheni cha IRIB cha Iran ni vya serikali na vinadhibitiwa na wahafidhina. ripoti nyingi ni za upande mmoja na zinathibisha mpango wa wahafidhina," msomi wa sayansi ya siasa Sadegh Zibakalam aliliambia shirika la habari la Deutsche Welle.
Harakati za mitandaoni zinachukuliwa kuwa kama makosa ya mitandaoni
Chini ya Uongozi wa rais wa sasa Hassan Rouhani, na hasa katika kufuatilia kukamilika kwa mpango wa ufanisi wa nyuklia, nchi hiyo pole pole imeanza kufunguka. katika kufunguka huku Iran na ubadilishanaji na ulimwengu wa nje ya Iran imeimarisha jamii ya umma na kazi zake ya elimu ya mtandaoni.
"Lakini sehemu chache tu ndio zinaonekana kupata faida mpaka sasa. Sehemu hizi ni zile ambazo haziwi na migogoro ya moja kwa moja na dhana ya maadili ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran," alisema muandishi wa habari Reza Haghighatnejad.
"Serikali imeona nguvu ya mitandao ya kijamii. Wanachama wake wote wanatumia mitandao hiyo, kutoka mkuu wa kiongozi hadi wagombea urais," anasema Haghighatnejad.
Muandishi huyu wa habari alisema pia kuwa wanasiasa hao wanatumia mitandao kusambaza malengo yao ya kisiasa, lakini bado wanapinga upatikanaji kamili wa utumiajiwa mitandao kwa watu wote.
" Hata hivyo, wamepoteza udhibiti wao taarifa," alisema muandishi wa habari na mwanaharakati Reza Haghighatnejat.
Mwandishi: Najma Said
Mhariri: Saumu Yusuf