Maafisa wa usalama mjini Nakuru, Kenya, wamewakamata wahubiri wawili raia wa Uganda kwa madai ya kuwasafirisha waumini kutoka Uganda kuelekea Ethiopia kwa njia isiyo halali. Polisi waliolazimika kuwarejesha raia 83 wa Uganda nchini kwao, wamelalamikia mianya kwenye mipaka ya Kenya.