Mashambulio ya "Dola la Kiislamu"
21 Mei 2015Gazeti la "Stuttgarter" linautilia maanani uamuzi wa Spika wa Bunge la Ujerumani kukataa kukutana na Rais wa Misri atakapofanya ziara nchini Ujerumani.
Spika wa Bunge la Ujerumani Nobert Lammert amekataa kukutana na Al -Sissi kama ishara ya kupinga kukiukwa haki za binadamu nchini Misri. Mhariri wa gazeti la "Stuttgarter" anautilia maanani uamuzi wa Spika huyo lakini anasema ni sahihi kwamba Rais wa Misri atafanya ziara nchini Ujerumani.
Magaidi wa "Dola la Kiislamu" waimarika
Mhariri huyo anasema,kuifuta ziara hiyo kungelikuwa na maana ya kujinyima fursa ya kutoa maoni juu ya yale yanayotokea nchini Misri. Mhariri wa "Mittelbayerische" anazunguzmia juu ya kuimarika kwa "dola la kiislamu" nchini Syria na Iraq.Na inaikosoa sera ya Obama juu yamagaidi hao.
Mhariri huyo anasema wakati "dola la kiislamu" linajitandaza na kujiimarisha nchini Syria na Iraq, Marekani inapata mafanikio ya hapa na pale. Kutekwa mji wa Ramadi na "dola la kiislamu" nchini Iraq, maana yake pia ni pigo kwa sera ya utawala wa Obama juu ya magaidi wa "dola la kiislamu." Kosa la utawala wa Obama inapohusu kuwakabili magaidi hao ni kuwategemea washirika ambao kwa kweli hawapo.
Mhariri wa gazeti la "Volksstimme" anatoa ushauri kwa Umoja wa Ulaya ikiwa unataka kujenga ushirikiano mwafaka na nchi za Ulaya ya Mashariki. Mhariri huyo anasema kutokana na yale yaliyotokea nchini Ukraine, litakuwa jambo la manufaa ikiwa Umoja wa Ulaya utaachana na dhana ya kuziona nchi za Ulaya Mashariki kama jumuiya moja.
Nchi hizo zinatafautiana kwa namna mbalimbali.Ndiyo sababu,kwamba Umoja wa Ulaya unapaswa kutiliana saini na kila nchi peke yake. Ushirikiano wowote baina ya Umoja wa Ulaya na nchi za Ulaya ya Mashariki unapaswa kuyazingatia maslahi ya Urusi. Inapasa kujifunza kutokana na yale yanayotokea mashariki mwa Ukraine.
Mwandishi:Mtullya Abdu.Deutsche Zeitungen.
Mhariri: Iddi Ssessanga