Matangazo
Hii ni baada ya rais Uhuru Kenyatta siku ya Alhamis kutia saini na kuufanya kuwa sheria mswada uliodhinishwa na bunge wiki iliyopita baada ya kuwasilishwa na mbunge Ken Okoth. Sheria hiyo mpya sasa inamaanisha waliotekeleza vitendo hivyo wanaweza kufungwa jela kwa miaka 15 au kutozwa faini ya shilingi milioni 2 pesa za Kenya. Kufahamu mengi kuhusu sheria hii mpya, DW imezungumza na mwanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu nchini Kenya Eric Karisa Mgoja.