Wahamiaji wa Kiafrika wafa maji katika bahari ya Shamu
4 Januari 2011Matangazo
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya ndani ya Yemen, kuna hofu kuwa hadi wakimbizi 80 kutoka Afrika wamepoteza maisha yao katika ajali ya boti mbili iliyotokea baharini wakati wa upepo mkali. Boti moja ilipinduka kusini mwa Bahari ya Shamu siku ya Jumapili, ikiwa na watu 46 na wengi wao, walikuwa Waethiopia. Wasomali 3 waliokolewa.
Ajali ya pili ilitokea karibu na mji wa Aden ulio kusini mwa Yemen. Boti hiyo ilikuwa na Waethiopia kati ya 35 hadi 40. Ripoti zinagongana kuhusu idadi ya watu waliokufa katika ajali hiyo. Kila mwaka, Waethiopia na Wasomali, kwa maelfu, husafiri njia hiyo ya hatari kwenda Yemen, kwa matumaini ya hatimaye kuelekea Saudi Arabia au nchi nyingine tajiri kutafuta kazi.