Mamlaka ya uhamiaji nchini Tanzania imewatia mbaroni wahamiaji haramu 110, katika operesheni yake ya kuwasaka raia wa kigeni wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria. Kati ya wahamaiaji hao waliokamatwa, 76 wamefikishwa mahakamani hii leo na wengine uchunguzi dhidi yao ukiendelea.