1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUhispania

Wahamiaji 5 wafariki wakijaribu kufika visiwa vya Canary

4 Novemba 2024

Miili mitano ilipatikana ikielea baharini Jumapili baada ya boti ya mpira inayofanya kazi kwa kutumia upepo waliyokuwa wakisafiria kutoboka umbali wa kilomita 90 kutoka kisiwa cha Lanzarote nchini Uhispania.

https://p.dw.com/p/4mYNq
Wahamiaji kutoka Afrika wakiwasili kutoka Uturuki kwa boti ya mpira kwenye ufuo wa kijiji cha skala Sikamias huko Lesbos.
Wahamiaji kutoka Afrika wakiwasili kutoka Uturuki kwa boti ya mpira Picha: Angelos Tzortzinis/picture alliance/dpa

Msemaji wa huduma za Uokoaji za Bahari ya Uhispania amesema ndege ya uokoaji iliona boti mbili zikielekea katika visiwa hivyo vya Canary na kwamba moja ilionekana kupungua hewa.

Watu 9 wamefariki baada ya boti yao kuzama karibu na Canary

Ndege hiyo ilirusha vifaa viwili vya kuokoa maisha na kuwaokoa watu 17 kutoka kwa boti moja na wengine 80 kutoka boti ya pili lakini miili mitano pia ilipatikana.

Watu 48 wafariki dunia wakijaribu kufika visiwa vya Canary

Wakati huo huo, imeripotiwa kwamba takriban wahamiaji 48 walikufa wakijaribu kufika katika Visiwa hivyo vya Canary kwa kutumia boti iliyoondoka Mauritania wiki tatu zilizopita.

Taasisi ya serikali EFE imesema, kwa ujumla, huduma za uokoaji ziliwaokoa zaidi ya watu 1500 mwishoni mwa wiki.