Wahamiaji 46 waokolewa katika bahari ya Mediterania
8 Julai 2023Matangazo
Taarifa ya shirika lisilo la kiserikali la SOS humanity iliyotolewa leo kupitia mtandao wa Twitter imesema, watu hao walijaribu kuingia Ulaya kwa kutumia boti ndogo miongoni mwao wakiwa wanawake wanne, mtoto wa kike wa miaka minne aliyekuwa akisafiri na baba yake na takriban watoto 10 ambao walisafiri pekeyao.
Wengi wa wahamiaji hao waliookolewa ni kutoka Eritrea, Ethiopia na Sudan. Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM linasema, mediterania ya kati ndiyo njia hatari zaidi ya wahamiaji duniani.
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limekadiria kuwa tangu mwanzoni mwa 2023, wahamiaji 1,728 wamepotea katika njia hiyo ikilinganishwa na 1,417 kwa mwaka mzima wa 2022.