Wahamiaji 40 wazama katika pwani ya Mauritania
7 Agosti 2020Matangazo
Mjumbe maalum wa UNHCR Vincent Cochetel ameandika kwenye mtandao wa Twitter kuwa boti hiyo imezama katika pwani ya Noaudhibou.
Cochetel ameongeza kuwa wameanzisha juhudi za kuzuia mikasa ya aina hiyo kutokea japo wanaofanya biashara ya kusafirisha wahamiaji wamekuwa wakiwahadaa wateja wao.
Wahamiaji wamekuwa wakitumia njia hiyo hatari kutoka Magharibi mwa Afrika hadi visiwa vya Canary ili kujaribu kutafuta maisha bora barani Ulaya.
Hata hivyo, idadi ya wahamiaji wanaojaribu kutumia njia hiyo kuingia Ulaya imepungua kwa kadri baada ya Uhispania kuanza kufanya doria katika miaka ya 2000 japo njia hiyo imeanza tena kutumika katika siku za hivi karibuni.