Wahamiaji 21 wakiwemo watoto 5 wafa katika bahari ya Aegean
15 Machi 2024Matangazo
Mtu mmoja alifanikiwa kujiokoa mwenyewe. Boti hiyo ilizama kwenye kisiwa kikubwa cha Uturuki cha Gokceada au Imbros kinachopatikana kwenye jimbo la Kaskazini Magharibi mwa Bahari ya Aegean la Canakkale.
Juhudi za uokoaji zinafanyika kwa msaada wa ndege moja, helkopita mbili, droni moja, boti 18 na maafisa wapatao 502. Uturuki inawahifadhi wakimbizi karibu milioni 4, wengi ni kutoka Syria.
Serikali mjini Ankara ilifikia makubaliano ya kupewa usaidizi wa kifedha na Umoja wa Ulaya mnamo mwaka 2016 ili kukabiliana na wimbi la wahamiaji wanaojaribu kuingia Ulaya.