1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 15 wafa maji Libya

12 Oktoba 2021

Wahamiaji 15 wamekufa maji baada ya mashua mbili kugonga mwamba kwenye pwani ya Libya.

https://p.dw.com/p/41ZPX
WS | Mittelmeer Sea-Watch 3 rettet Migranten vor Italien
Picha: Darrin Zammit Lupi/REUTERS

Huo ndio mkasa wa hivi karibuni kabisa wa wakimbizi wanaopoteza maisha wakisaka kuingia barani Ulaya.

Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, limesema miili ya watu hao 15 iliopolewa baada ya mashua mbili kuwasili kwenye Kituo cha Jeshi la Wanamaji mjini Tripoli jioni ya jana.

Shirika hilo limesema watu wengine 177 waliokolewa, ambapo kwa sasa wanahudumiwa na shirika hilo na washirika wake.

Tukio hilo ni sehemu ya mkururo wa matukio ya meli na mashua kuzama katika Bahari ya Mediterenia, ambapo wakimbizi wengi kutokea mataifa ya kusini mwa jangwa la Afrika wanapoteza maisha wakitaka kufika barani Ulaya.

Libya ni kituo muhimu cha kuondokea wahamiaji hao, ambapo maelfu hujazana kwenye mashua zisizo salama kuvuuka masafa ya kilomita 300 kufika pwani za Italia.

Kuanzia mwezi Januari hadi Agosti, wahamiaji 1,010 wameshapoteza maisha kwenye safari hizo.