1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 15 wa Ethiopia wapoteza maisha baharini

Yusra Buwayhid
31 Julai 2019

Raia wapatao 15 wa Ethiopia wamefariki baada ya boti waliokuwa wamepanda kuelekea Yemen kuharibika baharini.

https://p.dw.com/p/3N4Pc
Libysche Migranten ertrunken
Picha: picture-alliance/AP Photo/H. Ahmed

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wahamiaji limeripoti kwamba raia wapatao 15 wa Ethiopia wamefariki baada ya boti waliokuwa wamepanda kuelekea Yemen kuharibika na kuwaacha katikati ya bahari bila ya chakula wala maji kwa wiki nzima.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM limesema walionusurika wameeleza kwamba baadhi yao walifariki kutokana na njaa na kiu na wengine walijizamisha kusudi.

Wengine kadhaa waliwahi kufika nchini Yemen, lakini walifariki kabla ya kupata msaada wa matibabu.

Yemen imetumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miaka minne, lakini maelfu ya wahamiaji kutoka Pembe ya Afrika wanakwenda nchini humo kwa matarajio ya kuvuka mipaka na kuingia katika mataifa mengine tajiri ya Ghuba ya Kiarabu.