1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahafidhina wawashinda wapendeleao Ulaya uchaguzi Poland

8 Aprili 2024

Chama cha Waziri Mkuu Donald Tusk kinachopendelea muungano wa Ulaya kiko nyuma ya chama cha upinzani ambacho kilikuwa kinaitawala nchi hiyo kwa miaka minane hadi Disemba 2023.

https://p.dw.com/p/4eWWr
Waziri Mkuu wa Poland, Donald Tusk.
Waziri Mkuu wa Poland, Donald Tusk.Picha: Lukasz Gagulski/EPA

Ingawa matokeo ya mwisho yalikuwa yanatarajiwa mchana wa Jumatatu (Aprili 8), tayari chama cha kifadhidhina cha Law and Justice kilikuwa kiko mbele kwa asilimia 33.7 ya kura, kikifuatiwa na chama cha Waziri Mkuu Tusk, Civic Coalition, chenye asilimia 31.9.

Soma zaidi: Upinzani nchini Poland wafanya mkutano mkubwa wa kampeni

Uchaguzi huo wa Jumapili uliokuwa wa serikali za mitaa na majimbo unatazamwa kama kipimo cha kwanza kwa serikali ya mseto inayoongozwa narais huyo wa zamani wa Baraza Ulaya.

Kwa matokeo haya, inaonekana bado chama cha Law and Justice kimesalia kuwa na nguvu licha ya kuangushwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana.