1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahafidhina wapoteza wingi bungeni katika uchaguzi Bavaria.

Kitojo, Sekione29 Septemba 2008

Chama cha CSU kilichokuwa kinatawala peke yake katika jimbo la Bavaria kwa miongo kadha sasa hakitaweza kufanya hivyo tena baada ya kupata wingi mdogo wa kura na kuhuitaji mshirika.

https://p.dw.com/p/FQuU
Waziri wa zamani wa kazi katika serikali ya mseto kati ya chama cha kansela wa Ujerumani Angela Merkel cha CDU na SPD Franz Muenterfering katika mkutano wa kampeni mjini Munich hivi karibuni.Picha: AP


Katika jimbo la Bavaria nchini Ujerumani , chama cha kihafidhina cha CSU ambacho kimekuwa kikitawala peke yake tangu miongo kadha kimeshindwa kulinda ushindi wake huo usiporomoke. Chama hicho kimeanguka kutoka asilimia 60.7 ilizokuwa imepata katika uchaguzi uliopita miaka mitano iliyopita hadi kiasi cha asilimia 43.4 na sasa kinahitaji kutawala kwa kukishirikisha chama kingine. Chama cha FDP kinaonekana kuwa tayari kuwa mshirika wa chama hicho katika serikali ya mseto katika jimbo hilo.


Katika makao makuu ya vyama vyote vilivyoshiriki katika uchaguzi huo mjini Munich furaha ilikuwa kubwa zaidi katika chama cha FDP kuliko pengine. Chama hicho cha kiliberali baada ya kushindwa vibaya mara tatu katika uchaguzi wa jimbo la Bavaria ni dhahiri kilikuwa kinatarajia kurejea tena, na kutumai kuwa chama cha CSU ambacho kimekuwa kikitawala peke yake kwa muda wa karibu nusu karne kitapoteza madaraka hayo. Na aliyekuwa na furaha zaidi alikuwa kiongozi wa chama cha FDP Guido Westerwelle ambaye amesema kuwa hivi sasa kwa mara nyingine tena tunauwakilishi imara katika majimbo 13 Ujerumani nzima. Hii ina maana kwamba kwa mara nyingine tena , katika Ujerumani FDP ni nguvu ya tatu, na hii imeonekana tena katika uchaguzi huu wa majimbo.Chama cha Christian Social Union CSU kimepoteza wingi wake katika bunge la jimbo la Bavaria, siku ya Jumapili , hii ikionekana kama jaribio la uungwaji wake mkono kabla ya uchaguzi mkuu wa taifa mwaka ujao. Matokeo yanaonyesha upungufu wa asilimia 17 kutoka wingi ambao chama hicho kimezowea kupata katika chaguzi zilizopita na kulazimisha chama hicho kutafuta mshirika wa kuweza kuunda serikali.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekabiliwa na ukosoaji baada ya wahafidhina kupoteza kwa wingi uchaguzi huo , huku chama hicho ndugu ya chama cha kansela kushutumu sera zake katika muungano mkuu wa serikali kwamba ndio uliosababisha kuanguka huko , licha ya kuwa katibu mkuu wa chama cha CSU Ronald Pofalla , anaona kuwa katika kuanguka huko chama chake bado kinamatumaini.

Kura ambazo CSU imepoteza zinabaki katika hali ya wapigakura wa Bayern. Wapiga kura wametoa tahadhari ya kutaka mabadiliko. CSU , FDP na wanaojitegemea kwa pamoja wamepata kiasi cha zaidi ya asilimia 60.


Hata chama cha SPD ambacho kimo katika serikali ya mseto inayoongozwa na chama cha kansela Angela Merkel cha CDU hakikufaidika na kuporomoka kwa chama cha CSU na wameporomoka nao kwa moja asilimia na kufanikiwa kupata asilimia 18.6. Chama cha SPD kiliweka matumaini yake kutoka na kumteua mwezi huu waziri wa mambo ya kigeni Frank-Walter Steinmeier kuwa mgombea wa kiti cha ukansela dhidi ya Merkel mwezi Septemba 2009 katika uchaguzi mkuu na kumteua Franz Muentefering kuwa mwenyekiti wake wa chama ili kukipa nguvu mpya.

Uongozi huo mpya wa Steinmeier na Muentefering haukuweza kuwashawishi zaidi wapiga kura. Lakini licha ya kuporomoka huko Steinmeier alikuwa pia na matumaini na kueleza kuwa

huu ni utamaduni mpya wa kisiasa katika jimbo la Bayern na utatusaidia.

Matokeo hayo yanauweka muungano unaounda serikali unaongozwa na Merkel ukiwa katika mwaka wake wa tatu sasa katika hali ngumu katika uchaguzi ujao , hususan kutokana na kupata nguvu kwa vyama vidogo kama ilivyoonekana katika uchaguzi wa Bavaria jana Jumapili, ikiwa na maana kuwa hali hiyo inaweza kuendelea hadi katika uchaguzi mkuu ujao mwakani.




►◄