Waguinea Bissau wasubiri matokeo ya uchaguzi
5 Juni 2023Kwa mujibu wa kituo cha demokrasia na maendeleo ambalo ni shirika la kutetea haki za binadamu Afrika, takriban watu milioni 1 walijiandikisha kupiga kura kuchagua zaidi ya wabunge 100 kutoka vyama 6 vya kisiasa.
Rais Umaro Sissoco Embalo aliyewahi kuwa jenerali wa jeshi aliingia madarakani Desemba mwaka 2019 baada ya kushinda duru ya pili ya uchaguzi lakini akanusurika jaribio la kumpindua madarakani Februari mwaka 2022 lililofanywa na kundi lililokuwa na silaha liliishambulia ikulu.
Soma pia: Guinea-Bissau:ECOWAS imelitolea mwito jeshi kubaki kando na siasa
Wachambuzi wanasema tangu kuingia kwake madarakani amekuwa akikandamiza uhuru wa kiraia wakati taasisi za kiserikali zikipoteza uhuru. Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa siku chache zijazo.