1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagombea wa upinzani wauawa katika uchaguzi Tanzania

28 Novemba 2024

Chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania kimeripoti kuwa wanachama wake watatu wameuawa katika matukio yanayohusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa, na kuwatuhumu maafisa kukiibia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM).

https://p.dw.com/p/4nVRi
Tanzania | Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman MbowePicha: Ericky Boniphace/DW

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alisema kupitia mtandao wa X kuwa mgombea Modestus Timbisimilwa alipigwa risasi na polisi jijini Dar es Salaam alipojaribu kuzuia kura bandia, wakati mgombea mwingine, George Juma Mohamed, aliuawa na maafisa wa magereza huko Mkese wakati wa vurugu, huku Steven Chalamila, akiripotiwa kuuawa kwa shambulio la panga nyumbani kwake Tunduma.

Soma pia: Mchungaji Peter Msigwa wa CHADEMA ajiunga na CCM

Mbowe alisema wanaamini matukio hayo yamefanywa kwa baraka na idhini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Tanzania ilichagua zaidi ya viongozi 80,000 wa serikali za mitaa, ambao wana mamlaka makubwa katika taifa hilo. Uchaguzi huo ni mtahani mkubwa kwa vyama na taasisi za kidemokrasia nchini humo, kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka ujao.

CCM, ambayo imetawala siasa za Tanzania kwa miongo kadhaa, ilituhumiwa kwa ongezeko la ukandamizaji na kuwaengua wagombea wa Chadema kwa njia zisizo haki, sawa na uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2019 ambapo Chadema waligomea kutokana na vurugu na vitisho.