1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Wagner yadai kukamata eneo lote la mashariki mwa Bakhmut

8 Machi 2023

Mkuu wa kampuni ya mamluki ya Urusi, Wagner amesema kuwa wapiganaji wake wameikamata sehemu yote ya mashariki ya Bakhmut, mji wa mashariki mwa Ukraine ambako mapigano yamerindima kwa wiki kadhaa.

https://p.dw.com/p/4OOBZ
Ukraine | Krieg | Videostill Wagner-Chef Jewgeni Prigoschin
Picha: Konkord Company Press Service/ITAR-TASS/IMAGO

Mkuu wa kampuni ya mamluki ya Urusi, Wagner amesema kuwa wapiganaji wake wameikamata sehemu yote ya mashariki ya Bakhmut, mji wa mashariki mwa Ukraine ambako mapigano yamerindima kwa wiki kadhaa. Yevgeny Prigozhin amesema katika ujumbe wa sauti uliotolewa na kitengo chake cha habari kuwa vikosi vyake vimekamata eneo lote la mashariki la mto wa Bakhmut linalougawa mji huo. Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu amesema kukamatwa Bakhmut kutadhoofisha zaidi ngome za Ukraine na kuiwezesha Urusi kufanya mashambulizi zaidi katika eneo la Donbas, kunakopatikana majimbo ya Donetsk na Luhansk ambayo Urusi inasema inapigana kuyakomboa.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Ukraine itaendelea kuupigania mji huo, wakati kukiwa na tetesi kuwa askari wa Ukraine wanaweza kujiondoa. Waziri wa Ulinzi wa Marekani Llyod Austin amepuuza umuhimu wa kimkakati wa mji huo, akisema kukamatwa kwake kutakuwa tu ni ushindi wa kiishara na hakutabadilisha mkondo wa vita.