1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waganda 211 wawasili nyumbani kutoka Sudan

Emmanuel Lubega27 Aprili 2023

Raia wa Uganda wapatao 211 wamewasili nyumbani mkesha wa leo wakitokea Sudan, walikokuwa wamekwama kufuatia kuzuka kwa mapigano nchini humo wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/4Qcsw
Sudan | Flucht nach Ägypten
Picha: - /AFP/Getty Images

Imekuwa furaha na nafuu kwa raia hao wa Uganda pamoja na jamaa zao waliowasubiri kwa muda wa siku tatu tangu walipopata habari kwamba wameanza safari kutoka Khartoum. Awali Uganda ilipanga kuwanusuru raia wake 300 lakini ni  211 tu waliowasili ikiwemo wanafunzi, wafanyabiashara, maafisa wa ubalozi na mahujaji waliokuwa wanaelekea Makka.

Soma pia: Sudan: Mkuu wa majeshi aashiria kulikubali pendekezo la IGAD la kuongeza muda wa kusitisha mapigano

Balozi wa Uganda nchini Sudan Dkt. Rashid Yahya Ssemuddu ambaye alipewa jukumu na rais Museveni kuhakikisha kuwa raia hao wanashughulikiwa ipasavyo amesema.

Evakuierung Indonesische Bürger aus dem Sudan
Serikali za magharibi zimekuwa zikiwahamisha raia waoPicha: MOFA RI

Wakisimulia madhila yao baadhi ya raia wa Uganda wanaelezea kuwa hali ya mapigano nchini Sudan ni ya kusikitisha zaidi na wanamshukuru Mungu kwamba waliweza kunusurika. Wanasimulia kuhusu safari ndefu waliofanya tangu Jumatatu walipoondoka Khartoum wakisafiria barabara kwa takriban saa 13 kabla kufika mji wa mpaka wa sudan na Ethiopia wa Garabati. Ndege iliyopangwa kuwapokea haingeweza kutua uwanja wa ndege  wa Gondo na ilibidi wasafirishwe hadi uwanja wa Bahar walikoabiri ndege kurudi nyumbani. Baadhi yao wanasema

Balozi amewaambia wanahabari kuwa Rais Museveni alifuatilia shughuli hiyo kila mara akitaka kuhakikishiwa kuwa kila kitu kinakwenda sawa.

Imefahamika kuwa angalau raia 80 wa Uganda hawangeweza kufanya safari hiyo ya mashaka na wamebaki Sudan chini ya ulinzi wa ubalozi na mashirika ya kimataifa. Mataifa kadhaa yameendelea kushirikiana katika juhudi za kuwanusuru raia hao waliokwama Sudan. Wakati huohuo, mwito umetolewa kwa pande zinazozozana kusitisha mapigano hayo ambayo hadi sasa yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 400 na wengine wengi kujeruhiwa. Lubega Emmanuel DW Kampala