1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafungwa wateswa kinyama Guantanamo

Sylvia Mwehozi
27 Juni 2023

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa waliotembelea gereza la Marekani la Guantanamo wamewasilisha ripoti inayoelezea matendo ya kinyama dhidi ya wafungwa.

https://p.dw.com/p/4T6ci
USA Kriminalität l Behandlung von Guantánamo-Insassen l Camp 5 Außenansicht
Picha: Thomas Watkins/AFP

Kwenye ripoti yao waliyoiwasilisha siku ya Jumatatu (Juni 26), wataalamu hao wamesema mazingira ya wafungwa 30 wa mwisho katika gereza hilo ni ya kikatili, kinyama na udhalilishaji. 

Mwandishi maalumu wa Umoja wa Mataifa, Fionnuala Ni Aolain, alisema dhuluma katika gereza hilo ni sawa na ukiukwaji wa haki za kimsingi na uhuru wa wafungwa.

Wafungwa hao wanashikiliwa kwa takriban miongo miwili baada ya kukamatwa kama washukiwa kufuatia mashambulizi ya al-Qaida nchini Marekani mwaka wa 2001.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa walilitembelea gereza la Guantanamo mnamo mwezi Februari.