1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafungwa waanzisha mgomo wa njaa Misri

Yusra Buwayhid
31 Julai 2019

Takriban wafungwa 130 wamekuwa katika mgomo wa njaa katika gereza moja la Misri kwa zaidi ya wiki sita wakilalamika juu ya hali mbaya ya kibinadamu.

https://p.dw.com/p/3N4Pw
Ägypten Tora Gefängnis nach dem Tod von Mohammed Mursi
Picha: Reuters/A.A. Dalsh

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu Amnesty International limesema leo kwamba wafungwa wapatao 130 wamekuwa katika mgomo wa njaa katika gereza moja la Misri kwa zaidi ya wiki sita wakilalamika juu ya hali mbaya ya kibinadamu na kukataliwa kuonana na familia zao.

Wengi wa wanaoshiriki mgomo huo wa njaa katika gereza la ulinzi mkali la kusini mwa Cairo la Al-Agrab walikamatwa zaidi ya miaka miwili iliyopita na hawakuwahi hata mara moja kuruhusiwa kutembelewa na familia za au wanasheria wao.

Shirika hilo limenukuu tamko lilotlewa na wafungwa na kusema kwamba tangu mgomo huo kuanza mnamo Juni 17, walinzi wa gereza hilo waliwawaadhibu wafungwa hao kwa kuwapiga, pamoja na kutumia mshtuko wa umeme.

Makundi ya kutetea haki za binadamu mara kwa mara yanaukosoa utawala wa Rais Abdel Fattah al-Sisi, uliochukua madaraka mwaka 2013 baada ya kumuondoa Mohammed Morsi, kwa kuwanyamazisha wapinzani wake.