Nchini Uganda, jamaa mmoja ameanzisha mpango wa chakula cha kuku na hivyo kuwapunguzia wafugaji gharama kubwa ya chakula. Uganda ni kati ya nchi 10 za Afrika ambazo ufugaji wa kuku unatarajiwa kukua kwa asilimia 10. Hiyo ni kulingana na ripoti ya mwaka 2018 kutoka benki ya Rabo. Wakati ukuaji huo ukiendelea, jamaa huyu anapanaga kutumia lishe ya bei nafuu lakini yenye utajiri wa virutubisho.