1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Wafuasi wa Imran Khan waandamana kushinikiza atolewe jela

9 Septemba 2024

Maelfu ya wafuasi wa Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan aliye gerezani Imran Khan walikusanyika kwenye viunga vya mji mkuu Islamabad jana Jumapili kushinikiza mwanasiasa huyo aachiwe huru.

https://p.dw.com/p/4kPhQ
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan aliye gerezani Imran Khan.Picha: K. M. Chaudary/AP Photo/picture alliance

Khan yuko gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja kutokana na kesi zaidi ya 150 zilizofunguliwa na mamlaka za nchi hiyo.

Mkusanyiko huo wa jana ambao ni moja kati ya ile mikubwa kabisa iliyoandaliwa na chama cha Khan cha Tehreek-e-Insaf ulifanyika kwa amani ingawa kulitokea purukushani kidogo kati ya polisi na wanaharakati.

Polisi ilijaribu kuwazuia wafuasi wa Khan kuhudhuria mkusanyiko huo kwa kupanga makontena barabarani.

Khan, mpinzani mkuu wa Waziri Mkuu wa sasa Shebaz Sharif amebakia kuwa mwanasiasa mashuhuri nchini Pakistani licha ya kesi zinazomwandama ambazo wakosoaji na chama chake wanasema zimechochewa kisiasa.