1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafuasi wa al-Qaeda wakamatwa

29 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUPI

Wizara ya mambo ya ndani nchini Saudi Arabia imetangaza kuwa imewakamata zaidi ya wanamgambo 200 walio na mafungamano na kundi la kigaidi la al-Qaeda, wanaoshukiwa kuwa na njama ya kukishambulia kituo cha mafuta, mashehe na maafisa wa usalama.

Washukiwa hao walitiwa mbaroni katika harakati kubwa zaidi dhidi ya ugaidi kuwahi kufanywa nchini Saudi Arabia.

Kiongozi wa al- Qaeda, Osama bin Laden, ni mzaliwa wa Saudi Arabia na wafuasi wake wamekuwa wakijaribu kuwashambulia raia wa kigeni na biashara zao katika ufalme huo tangu mwaka wa 2003.