Wafanyakazi WFP washtushwa, kufurahishwa na tuzo ya Nobel
9 Oktoba 2020Kuanzia kudondosha chakula kutoka angani nchini Sudan Kusini, hadi kuunda huduma ya usafirishaji wa dharura ili kuendeleza utoaji wa msaada licha ya vizuwizi vya usafiri vya janga la virusi vya corona, shirika hilo lenye makao yake makuu mjini Rome, Italia, limejikita kwa muda mrefu katika kufikisha msaada kwa baadhiya maeneo hatari zaidi duniani.
Mwaka uliyopita, WFP ilitoa msaada kwa karibu watu milioni 100 katika matifa 88.
Soma zaidi: Shirika la Chakula Duniani WFP lashinda Tuzo ya Amani, Nobel
Kansela Merkel amesema iwapo shirik lolote linastahili tuzo hiyo, basi shirika hilo ni WFP. Akizungumza na waandishi habari mjini Berlin, Merkal ameongeza kuwa wafanyakazi wa shirika hilo wanafanya kazi ya kipekee kuwasaidia wengine, na kwamba amefurahia tuzo hiyo.
"Watu huko wanafanya isiyoaminika na wanasaidia watu wengine. Na kwa hivyo nimefurahi sana kwa kutolewa tuzo ya Nobel ya Amani." aliongeza Kansela wa Ujerumani.
Naye waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas katika ujumbe wake baada ya kutangazwa kwa tuzo hiyo, ametuma ujumbe wa kulipongeza shirika hilo na mkurugenzi wake David Beasley, na kusema juhudi za shirika hilo zinaokoa mamilioni ya maisha ya watu kutokana na njaa na utapiamlo kila siku. Ujerumani ni mfadhili wa pili kwa ukubwa wa WFP.
Mwenyekiti wa Nobel kuhusu sababu za kuichagua WFP
Mwenyekiti wa Kamati ya Nobel Berit Reiss-Andersen, ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba ingawa WFPingeshinda tuzo hiyo kutokana na kazi yake, 2020 ulikuwa mwaka ambamo njaa inaongezeka, na njaa inayohusiana na vita na mizozo pia inaogezeka.
"Hali ya dunia hivi sasa imetilia mkazo umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa. Na bila shaka hilo linahusu pia janga linalotukabili kwa sasa. Na njaa, kama ilivyo kwa janga, inatilia mkazo umuhimu wa kuwa na suluhu kwa changamoto za kidunia," alisema Berit.
Soma pia: Shirika la WFP laonya kuhusu njaa Msumbiji
Katibu Mkuu wa Umpja wa Mtifa Antonio Guterres amesema amefurahia kuona kwamba tuzo hiyo imeenda kwa muitikiaji wa kwanza duniani kwenye uwanja wa ukosefu wa usalama wa chakula.
Hii ndiyo tuzo ya 12 ya Amani ya Nobel kutolewa Umoja wa Mataifa, moja ya mashirika yake au watumishi - ikiwa ni idadi kubwa zaidi kuliko mpokeaji mwingine yeyote. Mwenyekiti wa kamati ya Nobel Reiss Andersen, amesema mashirika ya Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kimataifa zinaonekana kuwa na uungwaji mkono mdogo siku hizi, akitolea mfano wa mchakato wa Brexit na ukosoaji wa Marekani.
Wafanyakazi waelezea mushtuko, furaha
Wanahatarisha misha yao kulisha mamilioni ya watu katika baadhi ya meneo hatari zaidi duniani, lakini Ijumaa ilitoa fursa kwa wafanyakazi wa WFP kuhisi utambuzi fulani kwa kazi yao.
"Kwanya kabisaa kila moja alipatwa n mshutuko, na sasa wamezidiwa kidogo na kila kitu," alisema mkurugenzi mkaazi wa WFP nchini Sudan Kusini Matthew Hollingworth.
Soma pia: WFP kutuma tani 50,000 za ngano huko Lebanon
Sudan Kusini ni moja ya operesheni kubwa zaid za kibinadamu za WFP, wafanyakazi wake 1,200 walioko nchini humo wanahudumia watu wapatao milioni tano -- karibu nusu ya wakaazi wote -- katika taifa ambako njaa ya maksudi inatumiwa kama silaha ya kivita, na baa la njaa lintoa kitisho cha mara kwa mara.
Ni nchi pekee ambako WFP bado inadondosha chakula kutoka kwenye ndege kutokana na mzozo usiyoisha na ugumu wa kuizunguka nchi hiyo kubwa. "Wafanyakazi wamefurahi. Hilo halina mjadala," alisema Hollingworth kuhusu tuzo hiyo. "Najivunia kufanya kazi nao, kusema kweli."
"Niliposikia habari hizi...Niliacha kupumua, Sikuamini," alisema Espinola Caribe kutoka ofisi ya WFP nchini Msumbiji, ambako wamekuwa wakifanya kazi ya kuzihudumia jamii zilizoathiriwa na kimbunga kikali mwaka uliyopita.
Soma pia: Mamilioni kukumbwa na njaa kutokana na COVID-19
Alisema alitoka ofisi moja hadi nyingine, akiwapongeza na kuwashukuru wafanyakazi wake 50. Caribe aliezea ziara ya kikazi wiki iliyopita katika maeneo yalioathiriwa na kimbuga. "Ni hisia ambayo huwezi kuielezea, laazima uishi nayo, kuona namna watu wetu wanavyopambana kunusuru maisha ya watu."
Zaidi ya msaada wa chakula
Kazi ya WFP inakwenda mbali ya kutoa msaada wa chakula, na inahusisha kuzielimisha familia kuhusu liche ya watoto na kuwasadia kujitegemea.
Nchini Uturuki, ambako WFP inashirikiana na serikali na mashirika mengine kusadia wakimbizi wa Syria, shirika hilo limepanua huduma zake na kuanza kutoa programu za ufundi, likitoa mafunzo kwa Wasyria na Waturuki katik juhudi za kujenga mshikamano wa kijamii.
Soma pia: UN yasema watu milioni 820 wanakabiliwa na kitisho cha njaa
Katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, WFP inalisha watu wapatao 750,000 kila mwezi. Mkurugenzi wa mawasiliano wa WFP nchini humo, Vigno Hounkanli, amesema tuzo ya Nobel ni utambuzi wa kazi yote WFP iliyofanywa katika maeneo mengi tete zaidi.
Chanzo: Mashirika