1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na Haki

Wafanyakazi wa JKIA waliogama wakubali kurejea kazini Kenya

12 Septemba 2024

Chama cha wafanyakazi wa mamlaka ya safari za ndege kimeridhia kuumaliza mgomo na kurudi kazini baada ya mgomo wa siku nzima uliosababisha kukwama kwa shughuli za safari za ndege.

https://p.dw.com/p/4kWvl
 Nairobi uwanja wa ndege wa JKIA
Mgomo wa wafanyakazi wa JKIA umesababisha kuvurugwa kwa safari za ndege.Picha: Billy Mutai/AA/picture alliance

Wafanyakazi wa uwanja mkuu wa ndege nchini Kenya wamesitisha mgomo wao uliowakwamisha maelfu ya abiria, baada ya safari kadhaa za ndege kufutwa au kucheleweshwa.

Waziri wa usafiri wa Kenya Davis Chirchiri, amewaambia waandishi wa habari kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kufikia makubaliano na menejiment kuhusu utaratibu wa kurudi kazini.

Somam pia: Wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa JKIA nchini Kenya wagoma

Wanachama wa chama cha wafanyakazi wa ndege waligoma kuhusiana na mpango wa kukabidhi uendeshaji wa operesheni za uwanja huo kwa kampuni ya Adani ya India kwa kipindi cha maiaka 30, kwa kampuni hiyo kuwekeza dola bilioni 1.85.

Kiongozi wa shirikisho la vyama vya wafanakazi la Kenya, Francis Atwoli, amesema wamepatiwa nyaraka kuhusu uwekezaji huo, ambao wataupitia kabla ya kuamua hatua inayokuja. Mgomo huo ulioanza usiku wa manane uliathiri vibaya safari za ndege.