Mali: Wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu waachiwa huru
20 Machi 2023Taarifa ya ICRC iliyochapishwa jana jioni katika ukurasa wake wa Twitter, imeeleza kuwa wafanyakazi hao wako salama na wameachiwa bila masharti. Wafanyakazi wawili wa ICRC walitekwa nyara Machi 4, katika miji ya Gao na Kidal, kaskazini mwa Mali.
Nchi hiyo inakabiliwa na ukosefu wa usalama na mzozo wa kisiasa tangu mwaka 2012, wakati wapiganaji wa jihadi na makundi yanayotaka kujitenga yalipozuka kaskazini mwa nchi.
Soma pia: Makundi ya kigaidi nchini Mali yashambulia kambi ya jeshi
Daktari wa Shirika la Afya Duniani, WHO, alitekwa nyara nchini Mali mwishoni mwa mwezi Januari, na aliachiwa huru mwezi Februari.
Mwezi Mei, Waitaliano watatu na raia mmoja wa Togo walitekwa nyara kusini mwa Mali. Maelfu ya raia, polisi na wanajeshi wameuawa Mali na zaidi ya watu milioni mbili wameyakimbia makaazi yao.