Wafanyakazi nusu milioni moja wafanya mgomo mkubwa Uingereza
1 Februari 2023Matangazo
Muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini Uingereza (TUC) umeutaja mgomo huo kuwa mkubwa zaidi tangu mwaka 2011.
Walimu, madereva wa treni, maafisa wa mipakani, wa bandarini na viwanja vya ndege ni miongoni mwa wanaoshiriki.
Uingereza imekumbwa na migomo kwa miezi kadhaa, mnamo wakati mfumuko wa bei ya bidhaa nchini humo ukipita asilimia 11, hiyo ikiwa asilimia ya juu zaidi kwa zaidi ya miaka 40.
Bara la Ulaya linakabiliana na gharama ya juu ya maisha. Mgomo huo unajiri siku moja tu baada ya zaidi ya watu milioni 1.27 kuandamana nchini Ufaransa kushinikiza serikali kuhusu mipango yake ya mageuzi ya malipo ya uzeeni.