Mgomo wa kupinga sera za uchumi za Tinubu wafanyika Nigeria
5 Septemba 2023
Chama Kikuu cha Wafanyakazi nchini Nigeria, NLC, kinachowakilisha mamilioni ya watumishi wa sekta mbalimbali za taifa hilo la Afrika Magharibi ndiyo kimeratibu mgomo huo wa siku mbili kuanzia leo.
Chama hicho pia kinapanga kuongoza mgomo mwengine usio na kikomo kuanzia Septemba 21. Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na serikali ya rais Tinubu ambazo chama hicho inazipinga ni kufutwa kwa ruzuku ya mafuta ya petroli uamuzi uliosababisha kupanda kwa bei za nishati zaidi ya mara tatu.
Rais Tinubu akabiliwa na vihunzi lukuki katika safari yake ya mageuzi
Kiongozi huyo anasema hatua hizo hizo zinahitajika ili kuufufufa uchumi wa Nigeria na kuiwezesha nchi hiyo kulipa madeno. Hata hivyio viongozi wa chama cha wafanyakazi wameyataja mageuzi hayo kuwa "makali" na wamesema mgomo wao unataka kuona inisi serikali itaweza kubadili mwelekeo wa sera zake kwa sababu kila familia nchini humo imeguswa kwa ukali maisha.