1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waendesha mashtaka wakata rufaa dhidi ya hukumu ya Pistorius

4 Novemba 2014

Upande wa mashtaka umewasilisha rasmi rufaa dhidi ya hukumu ya kuua bila kukusudia na miaka mitano jela aliyopewa mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius kwa kumuua mchumba wake Reeva Steenkamp.

https://p.dw.com/p/1Dgis
Oscar Pistorius Gericht Pretoria
Picha: Reuters/M. Hutchings

Msemaji wa Idara ya Kitaifa ya Waendesha Mashtaka Nathi Mncube amesema hatua ya kukata rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa imetuwama katika suali la kisheria. Pistorius alikiri kumpiga risasi na kumuua Steenkamp nyumbani kwake mjini Pretoria, lakini akaiambia mahakama kuwa alidhania kulikuwa na mtu aliyevamia nyumba yake.

Jaji Thokozile Masipa wa Mahakama Kuu ya Pretoria hakuona ushahidi wa kutosha wa kumhukumu mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa kosa la kuua kwa kukusudia. Alipatikana na hatia ya kuua bila kukusudia na akahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA
Mhariri: Abdul-rahman