1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVisiwa vya Comoros

Wacomoro wasubiri matokeo ya uchaguzi wa rais

15 Januari 2024

Raia wa visiwa vya Comoro wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika siku ya Jumapili.

https://p.dw.com/p/4bF0r
Rais Assoumani anayechuana na wagombea wengine watano amesema anatumai kushinda katika duru hiyo ya kwanza ya uchaguzi.
Rais Assoumani anayechuana na wagombea wengine watano amesema anatumai kushinda katika duru hiyo ya kwanza ya uchaguzi.Picha: REUTERS

Rais aliye madarakani Azali Assoumani anatarajiwa kushinda muhula mwingine.

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea tangu kukamilika kwa upigaji kura jana jioni licha ya madai ya upinzani ya kuwepo kwa vitendo vya udanganyifu.

Kabla ya uchaguzi huo viongozi kadhaa wa upinzani kwenye taifa hilo la visiwa vya bahari ya Hindi, waliwatolea mwito wapiga kura kuususia.

Karibu wapinga kura 340,000 walikuwa wameandikishwa kushiriki uchaguzi huo kwenye taifa hilo lenye idadi kubwa ya waislamu na ambalo lilijitangazia uhuru kutoka ukoloni wa Ufaransa mnamo mwaka 1975.

Rais Assoumani anayechuana na wagombea wengine watano amesema anatumai kushinda katika duru hiyo ya kwanza ya uchaguzi.