Wachezaji wa Bundesliga watakaong'ara AFCON 2019
Michuano ya kuania kombe la mataifa barani Afrika-Afcon imeanza rasmi, Ifuatayo ni orodha ya wachezaji wanaokipiga ligi ya Bundesliga.
Achraf Hakimi (Morocco)
Licha ya umri wake mdogo, Hakimi alikuwa msaada wa kudumu katika klabu ya Borussia Dortmund. Kufuatia maumivu ya goti mwezi Aprili, ushiriki wake katika AFCON ulikuwa katika mashaka, lakini mchezaji huyo bora chipukizi wa mwaka wa Afrika, amepewa ruhusa ya kuingia uwanjani akiiwakilisha Morocco.
Ibrahima Traore (Guinea)
Mchezaji huyu wa Borussia Mönchengladbach ameonekana mara 11 katika msimu uliopita wa Bundesliga, kutokana na kusumbuliwa na upasuaji. Mshambuliaji huyu mwenye miaka 31, atakuwa nahodha wa Guinea na ameieleza Rheinische Post kuwa yuko fiti asilimia 100 na kwamba anakusudia kuliongoza taifa lake hadi hatua ya mtoano.
Salif Sane (Senegal)
Sane alikuwa msaada mkubwa kwa timu yake ya Schalke. Mlinzi huyu alicheza karibu kila mechi kwa upande wa Schalke na ana matumaini kwamba atakuwa msaada kwa timu yake ya Senegal.
Kasim Adams Nuhu (Ghana)
Wakati akijulikana katika Bundesliga kama Kasim Adams, lakini alijulikana kama Kasim Nuhu wakati alipoichezea timu ya vijana ya Bern ya Uswisi. Alishinda taji kabla ya kuhamia Hoffenheim. Jeraha alilopata mwanzoni mwa msimu lilitia wasiwasi wa kurejea uwanjani na hivyo alicheza mechi 13 za Bundesliga.
Amadou Haidara (Mali)
Mchezaji huyo mwenye miaka 21 ni miongoni mwa wachezaji kadhaa waliohama kutoka Red Bull Salzburg kwenda RB Leipzig mwezi Januari. Baada ya kuwasili Austria mwaka 2016, kiungo huyo wa kati alishinda taji la UEFA kwa vijana wa chini ya miaka 19 akiwa na timu ya Salzburg mwaka 2017, ukiwa ni mwaka ambao aliitwa katika timu ya taifa ya Mali.
Jean-Philippe Gbamin (Ivory Cost)
Kiungo huyo wa kati ataitumia michuano hiyo kama fursa ya kujiweka sokoni. Sio siri kwamba Gbamin, anatarajia kuachana na timu yake ya Mainz, msimu huu wa majira ya joto huku ligi ya England ikiwa ni matamanio yake. Hata hivyo amesema anaweza kuzichezea pia "Leverkusen au Dortmund."
Chadrac Akolo (DR Congo)
Mshambuliaji huyu wa Stuttgart alihamia Uswisi kama mkimbizi mwaka 2009 na wakati mmoja alifikiria kuiwakilisha nchi iliyompatia hifadhi badala ya DRC katika mechi za kimataifa. Katika msimu wa 2018-2019, Akolo alicheza michezo 16 ya Bundesliga, lakini hakufanikiwa kupachika goli na hivyo Stuttgart ilishuka daraja.
Simon Falette (Guinea)
Falette alizaliwa Ufaransa lakini ana asili ya Guinea. Maekuwa akichezea Eintracht Frankfurt tangu 2017, akicheza mara 29 katika msimu wa 2017-2018. Msimu uliopita alishuka lakini alicheza michezo 7 katika ligi ya Europa.
Cebio Soukou (Benin)
Inaweza isiwe Bundesliga lakini Cebio Soukou alipokuwa na miaka 18-19 alichezea timu ya daraja la tatu ya Hansa Rostock ya hapa Ujerumani. Aliitwa kikosini Benin miezi michache iliyopita. Msimu ujao ataichezea timu ya daraja la pili ya Arminia Bielefeld.
Manfred Starke (Namibia)
Mchezaji mwingine ni Manfred Starke ambaye amekuwa kwenye vitabu vya klabu ya FC Carl-Zeiss Jena tangu mwaka 2015. Starke, aliye na uraia pia wa Ujerumani, alijiunga na program ya vijana ya Hansa Rostock mwaka 2013 baada ya kuondoka Namibia. Kiungo huyo wa kati kushoto anaweza pia kucheza winga ya kushoto nyuma au katikati.
Marcel Tisserand (Congo)
Tisserand alikulia Ufaransa lakini aliamua kuiwakilisha Congo mwaka 2013. Alihamia Ujerumani mwaka 2016 na kujiung na Ingolstadt. Baada ya timu yake kushushwa daraja, alihamia Wolfsburg mwaka mmoja baadae na msimu ujao atacheza katika ligi ya Europa na timu ya Wolves.
Pierre Kunde Malong (Cameroon)
Licha ya kupokea elimu yake ya mpira wakati akisoma klabu ya Atletico Madrid, Kunde Malong hakuweza kupenya katika ligi ya Hispania. Baada ya kuwepo katika kikosi cha kwanza wakati wa mkopo katika klabu za Extremadura UD na Granada, mchezaji huyo mwenye miaka 23 alihamia klabu ya Mainz na kuonyesha uwezo mkubwa kiasi cha kujihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza.
Jamilu Collins (Nigeria)
Muda mfupi baada ya kutimiza miaka 18, Collins aliondoka Nigeria kuelekea Croatia alipojiunga na HNK Rijeka, na kisha kuuzwa kwa mkopo katika klabu nyingine za huko Croatia. Alijiunga na Paderborn 2017. Kiungo huyo wa kushoto huenda akaonekana Bundesliga kuanzia msimu ujao.
Mohamed Dräger (Tunisia)
Dräger hatokuwa mwakilishi pekee nchini Misri aliyeitwa kikosi cha Tunisia. Amezaliwa Freiburg na ameichezea SC Freiburg, amepitia timu ya vijana kabla ya kupata nafasi katika timu kubwa mwezi Julai 2017 na kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Europa dhidi ya NK Domzale. Ili aweze kucheza mara kwa mara, Dräger alinunuliwa kwa mkopo kwenda Paderborn 2018.