Hali nchini Libya inaendelea kuwa tete licha ya juhudi za kimataifa za kupatanisha makundi yanayohasimiana. Wakati juhudi hizo zikiendelea, ripoti ya hivi karibuni za Umoja wa Mataifa zinasema makundi ya mamluki yamekuwa yakihusika na mpango wa siri wa kumuunga mkono Jenerali Khalifa Haftar. Babu Abdallah alizungumza na mchambuzi wa siasa za kimataifa kutoka London Ahmed Rajab na kuhusu hili.