1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Wachambuzi wasema Al-Shabaab bado ni kitisho cha amani

22 Februari 2023

Wanamgambo wa Al-Shabaab nchini Somalia wanadai kuwaua takribani watu 10 baada ya kuvamia nyumba moja ya makaazi katika mji mkuu, Mogadishu ambapo baadhi ya wapiganaji wa kundi linaoiunga mkono serikali la Ma'awisley waliojeruhiwa walikuwa wakitibiwa.

https://p.dw.com/p/4Noxw

Wapiganaji wa kundi hilo walijeruhiwa katika mapambano na Al-Shabaab katika eneo la kati la Hiiraan. Vikosi vya usalama vya serikali ya Mogadishu vimesema mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijiripua muda mchache tu kabla ya wanamgambo hao waliokuwa na silaha kuvamia nyumba hiyo. Babu Abdalla amezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka kwenye mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Martin Oloo na kwanza alianza kuzungumzia malengo ya Al-Shabab pale wanapofanya mashambulizi ya aina hiyo.