SiasaSenegal
Wabunge watatu wa upinzani wakamatwa Senegal
7 Februari 2024Matangazo
Mvutano huo ni kufuatia hatua ya Bunge kupiga kura hapo jana na kuahirisha uchaguzi wa urais hadi Disemba 15 mwaka huu, hatua iliyotajwa na upinzani kuwa "mapinduzi ya kikatiba".
Miongoni mwa waliokamatwa ni mbunge Guy Marius Sagna ambaye alijaribu siku ya Jumatatu kuzuia zoezi la kuupigia kura mswada huo. Msemaji wa chama cha upinzani kilichofungiwa cha Pastef, El Malick Ndiaye amesema ni wazi sasa kwamba Senegal imeingia katika utawala wa kidikteta.
Hatua hiyo ya kuahirisha uchaguzi imesababisha maandamano makubwa katika miji kadhaa nchini Senegal pamoja na kuzua wasiwasi wa kimataifa kuhusu mustakabali wa nchi hiyo ambayo inachukuliwa kama kinara wa demokrasia huko Afrika Magharibi.