1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge wa Marekani wataka majibu vifo vya wanajeshi Niger

Sylvia Mwehozi
20 Oktoba 2017

Wabunge wa Marekani wanadai kupatiwa majibu wiki mbili baada ya shambulizi la kushutukiza lililotokea nchini Niger kuwaua wanajeshi wanne wa Marekani, huku mbunge mmoja akitishia kuliwasilisha suala hilo mahakamani.

https://p.dw.com/p/2mFZx
US Soldat  La David Johnson starb am 4. Oktober 2017
Picha: imago/Zumapress/Us Army

Ikulu ya Marekani imetetea kasi ndogo ya utoaji taarifa ikisema uchunguzi utatoa ufafanuzi wa kina juu ya janga hilo lililosababisha mgogoro wa kisiasa nchini Marekani.

Miongoni mwa maswali ambayo hayajaptiwa ufumbuzi ni, kwanini Wamarekani walishambuliwa kwa kushutukizwa? Kwanini ilichukua siku mbili za ziada ili kuupata mwili mmoja kati ya miili minne ya wanajeshi baada ya shambulizi kumalizikai?Je kundi la Dola la Kiislamu la IS lilihusika?.

Mgongono juu ya kile kilichotokea katika eneo la ndani la Niger ambako Wamarekani wachache husafiri, umezidi kumsakama rais Donald Trump ambaye alikuwa kimya juu ya vifo hivyo kwa zaidi ya wiki. Alipoulizwa kwa nini, Trump siku ya Jumatatu aliigeuza suala hilo kuwa ajenda ya kisiasa na kujisifu kwa kuwaenzi waliofariki na kuzifariji familia za wafiwa kuliko watangulizi wake. Alisema kwamba yeye binafsi alituma salamu kwa familia hizo lakini baadae baadhi ya familia zilizohojiwa zilikana kupokea salamu za Trump.

USA Donald Trump, Joseph L. Votel, Jim Mattis, H.R. McMaster, John Kelly, Paul Selva
Rais Donald Trump akipokea taarifa ya kiusalama Picha: picture-alliance/AP Photo/P.M. Monsivais

Katika taarifa isiyo ya kawaida kutoka Ikulu ya Marekani, John Kelly ambaye ni mkuu wa utumishi katika utawala wa Trump na Jenerali wa zamani wa jeshi la majini, alionyesha "kushangaa" na "kuvunjika moyo" na ukosoaji wa Trump. Pia alitaka mtoto wake wa kiume anayehudumu nchini Iraq na kuoa maelezo ya kwanini wanajeshi wa Marekani wanafanya kazi katika maeneo ya hatari duniani, akisema kwamba jitihada za kuwafunza wanajeshi wa ndani haimaanishi Marekani kufanya uvamizi mkubwa wenyewe. Mtoto wa Kelly mwingine, Robert aliuawa katika shambulizi nchini Afghanistan miaka saba iliyopita.

Shambulizi baya la kushutukiza nchini Niger lilitokea wakati wanamgambo wa kiislamu waliokuwa katika pikipiki, waliokuwa na maguruneti na silaha nzito  kuuvamia msafara wa Marekani na kupasua madirisha ya magari yasiyokuwa na ulinzi. Mbali na wanajeshi wanne waliouawa, wengine wawili walijeruhiwa. Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo. Shambulizi hilo kwa hivi sasa liko chini ya uchunguzi rasmi wa kijeshi.

Kwa mujibu wa seneta John McCain ambaye ni mwenyekiti wa Republican wa kamati ya seneti ya huduma za silaha, kinachoshangaza ni kasi ndogo ya utoaji wa taarifa. Seneta mwingine Mrepublican Bob Corker wa Tennessee ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya seneti ya mahusiano ya nje, amesema wabunge wamepewa baadhi ya taarifa juu ya shambulizi hilo, lakini sio wanazozitaka.

Katika wizara ya ulinzi, Pentagon, waziri wake Jim Mattis alisema inachukua muda kuthibitisha taarifa kuhusu shambulizi la kushutukiza. Ameahidi kutoa taarifa haraka iwezekanavyo pindi zitakapopatikana ingawa hakutoa tarehe rasmi. Mattis hakutoa maelezo ya mazingira ambako Wamarekani hao walipokuwa wakisafiri lakini alisema suala la kukutana na vikosi vya adui halikuzingatiwa.

Jim Mattis
Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim MattisPicha: Reuters/E. Vidal

Hilo linaweza kuelezea kwanini Wamarekani ambao walikuwa wakisafiri katika magari yasiyona usalama na wenzao wa Niger walikosa huduma za matibabu na huduma za ndege ingawa Mattis alisema waliwasiliana na Ufaransa na ndege yake ilikuja kwa haraka. Ndege hiyo iliibeba miili ya Wamarekani watatu, mwili wa mwanajeshi mmoja ulipatwa na wananchi wa Niger na ulirejeshwa Oktoba 6.

Mattis amesema Marekani ina wanajeshi 1000 katika eneo hilo la Afrika ili kuunga mkono ujumbe unaongozwa na Ufaransa wa kukabiliana na chembe za makundi ya itikadi kali. Ameongeza kwamba Marekani inatoa huduma ya ujazaji wa mafuta ndege angani, intelijensia na msaada wa utafiti wa kijeshi na vikosi vya ardhini ili kushirikiana na viongozi wa ndani.

"Katika kesi hii maalumu uwezekano wa kukutana na vikosi vya adui haukuzingatiwa, lakini sababu ya kwanini kulikuwa na wanajeshi wa Marekani pale na sio wafanyakazi wa kujitolea wa peace corps , ni kwasababu tunabeba silaha".

Kwa mujibu wa Mattis ujumbe unaotekelezwa na vikosi vya Marekani nchini Niger ni mfano wa hali ya juu wa mafunzo ambao jeshi la Green Berets limekuwa likufanya duniani kote kwa miongo kadhaa bila ya kufahamika.

Mwandishi: Sylvia Mwehozi/AP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman