Wabunge wa Kenya waridhia ijiondoe kwenye mkataba wa Roma
23 Desemba 2010Hatua hiyo inaonekana kama jaribio la kuidhinisha kusikizwa kesi dhidi ya washukiwa 6 wanaodaiwa kuhusika na ghasia baada ya uchaguzi mkuu uliopita nchini humo.
Mivutano ilijitokeza katika muungano tawala kwasababu ya suala la kuwatia hatiani watuhumiwa walioipanga njama iliyosababisha ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu uliopita.Baadhi ya wabunge hao wanataka Kenya ijiondoe kwenye mkataba wa Roma uliyoiunda mahakama ya ICC.Hali hiyo imekuwa bayana baada ya baraza la mawaziri kutangaza kuwa ina mpango wa kuzindua mahakama maalum itakayotumiwa kusikizwa kesi hizo za uhalifu.
Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC Louis Moreno Ocampo aliyawasilishia rasmi kwa majaji wa mahakama hiyo, majina ya watuhumiwa waliopanga njama iliyosababisha ghasia baada ya uchaguzi mkuu.Uchaguzi huo ulifanyika mwishoni mwa mwezi wa Disemba mwaka 2007.Miongoni mwa waliotajwa ni Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta na Waziri wa zamani wa Elimu ya ngazi za juu William Ruto.
Mwandishi: Halima Nyanza
Mhariri: Josephat Charo