SiasaJapan
Wabunge Japan wampigia kura Ishiba kuendelea na uwaziri mkuu
11 Novemba 2024Matangazo
Wabunge wamemteua Ishiba kuwa waziri mkuu wa serikali ya wachache, hatua inayomuweka katika hali ya msukosuko wa kisiasa au kuhitaji maelewano zaidi ili kupitisha miswada mipya.
Soma pia: Waziri Mkuu wa Japan Shigeru Ishiba aahidi kufanya "mageuzi ya msingi"
Ishiba, aliye na umri wa miaka 67 na waziri wa zamani wa ulinzi, aliingia madarakani wiki sita zilizopita na kufanya uchaguzi wa mapema mnamo Oktoba 27.
Soma pia: Muungano tawala Japan wapoteza wingi wa viti bungeni
Alikuwa na matumaini ya uungwaji mkono mkubwa kama kiongozi wa chama cha kihafidhina cha Liberal Democratic, LDP. Ishiba aliingia madarakani kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Fumio Kishida, aliyeng'atuka kufuatia kashfa ya ufisadi.