Wabunge Afrika Kusini wanataka ufugaji wa simba usitishwe
27 Novemba 2018Wabunge nchini Afrika Kusini wanataka kusitisha ufugaji wa simba kwa ajili ya uwindaji pamoja na kufanya biashara ya mifupa yao, na kuliweka bunge katika mvutano na wafanyabiashara wenye nguvu wa shughuli hiyo.
Afrika Kusini ina zaidi ya simba 8,000 wanaofugwa ambao wanazalishwa kwa ajili ya kuwinda, biashara ya mifupa yao, utalii na kwa ajili ya shughuli za utafiti, kwa mujibu wa makadirio ya makundi ya hifadhi ya wanyama.
Kwa ulinganisho kuna simba 3,000 wanaoishi porini wanaoishi katika mbuga za taifa ambako uwindaji umepigwa marufuku.
Kamati ya wabunge inayohusika na masuala ya mazingira imependekeza Novemba 12 kwamba serikali ifikirie upya kuhusu sheria zinazohusiana na uzalishaji wa simba wanaofugwa kwa ajili ya uwindaji na biashara ya mifupa yao.