Waasi wauwa wanajeshi 22 wa Niger
7 Oktoba 2016Matangazo
Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) umethibitisha kwamba kiasi cha watu 30 hado 40 waliokuwa na silaha wakizungumza lugha ya Kituareg walifanya mashambulizi hayo, ambapo wanajeshi 22 waliuwawa kwenye kambi hiyo iliyopo eneo la Tazalit jimbo la Magharibi la Tahoua nchini Niger.
Taarifa pia zimeeleza kwamba wanajeshi waliopelekwa katika eneo hilo baada ya shambulizi hilo walipambana na wapiganaji hao waliovuka mpaka na kurudi nchini Mali.
UNHCR inasema wanajeshi watano pia walijeruhiwa kwenye mashambulizi hayo, huku wengine watatu wakifanikiwa kukimbia.