Waasi wahujumu Somalia
18 Novemba 2007Matangazo
MOGADISHU:
Waasi wa kisomali wanaoipinga serikali wamewahujumu wanajeshi wa kuhifadhi amani wa umoja wa Afrika waliopo Somalia mjini Mogadishu.
Katika hujuma hiyo muasi mmoja aliuwawa baada ya vikosi vya Umoja wa afrika kurejesha mashambulio.Hujuma ya waasi imekuja siku 2 baada ya kiongozi wao Sheikh Aden Hashi Ayrow kuwaamru wapiganaji wake kulishambulia jeshi la amani la Umoja wa afrika liliopo Somalia.Sehemu kubwa ya jeshi hilo limechangiwa na wanajeshi wa Uganda.