Mratibu wa mpango wa kuwaondoa kutoka msituni wapiganaji wa makundi ya waasi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Tommy Tambwe amewasili mjini Beni kutathmini hali pamoja na kuzungumza na wadau watakaosaidia kuwashawishi waasi wakabidhi silaha kwa serikali. Beni inakabiliwa na mauaji na uharibifu unaodaiwa kufanywa na kundi la ADF la Uganda. John Kanyunyu alituarifu zaidi.