1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi nchini Mali wadai kuwakamata baadhi ya wanajeshi

20 Septemba 2023

Muungano wa wanamgambo waliojihami kwa silaha umesema umewakamata baadhi ya wafungwa wa kijeshi na kuwaua raia wengi katika operesheni ya hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/4WbaR
Jeshi la Mali limesema wanajeshi wake watano waliuawa na wengine 11 hawajulikani walipo
Jeshi la Mali limesema wanajeshi wake watano waliuawa na wengine 11 hawajulikani walipoPicha: SOULEYMANE AG ANARA/AFP/Getty Images

Aidha muungano huo umesema wapiganaji wake wanane pia wameuawa na wengine 12 kujeruhiwa.

Muungano huo wa vuguvugu la Azawad , CMA ambao unaundwa  na makundi ya waasi wa Kituareg wanaopigania kujitenga kwa eneo la Kaskazini mwa Mali aidha umedai kuzidungua ndege mbili katika shambulizi la Jumapili kwenye kambi mbili za kijeshi.

Jeshi la Mali limesema wanajeshi wake watano waliuawa na wengine 11 hawajulikani walipo, na kukiri kupoteza ndege zake, lakini likisema limewaua zaidi ya washambuliaji 30.

Lakini kundi hilo la wanamgambo limesema zaidi ya wanajeshi 35 waliuawa pamoja na rubani wa ndege na wengi kujeruhiwa na kudai kuchukua udhibiti kamili wa makambi siku ya Jumapili kabla ya kuondoka siku ya Jumatatu.