1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi Libya waingia Zawiyah

14 Agosti 2011

Mwandishi mmoja wa shirika la habari la Reuters aliyepo mjini Zawiyah nchini Libya ameeleza kuwa wapiganaji waasi wamelidhibiti eneo la kati la mji huo wa Zawiyah, kiasi ya kilomita 50 magharibi mwa mji mkuu wa Tripoli

https://p.dw.com/p/12GHc
Wapiganaji waasi LibyaPicha: Picture-Alliance/dpa

Mwandishi huyo ameeleza kuwa ameona kiasi ya waasi 50 karibu na soko kuu la Zawiyah wakipiga kelele wakisema, 'Mungu ni Mkubwa', huku bendera ya waasi ikipeperushwa katika duka moja.

Libyen Moussa Ibrahim 13. August 2011
Msemaji wa serikali Libya Moussa IbrahimPicha: dapd

Hatahivyo, utawala wa Gaddafi umelikana hili na kwa mujibu wa msemaji wa kiongozi huyo wa Libya, Mussa Ibrahim, vikosi vya Gaddafi bado vinaudhibiti mji huo.

Musa alieleza kuwa Bado kilichofanyika ni kuwa kundi dogo sana la waasi lilijaribu kusogea kusini mwa Zawiyah. Walikuwa chini ya waasi 100, ambao walisitishwa kwa urahisi na vikosi vyao vilivyojihami.

Waasi hao wameiambia Reuters bado kuna vikosi vinavyomtii Gaddafi mjini humo, wakiwemo wadenguaji risasi. Milio ya risasi ilisikika kwa kiasi, lakini hapakuwa na mapigano makali. Waasi hao wamesema kuwa sasa wanaulenga mji mkuu wa Tripoli.

Mwandishi: Maryam Abdalla/afpe, rtre
Mhariri:Othman Miraji